Thursday, March 3, 2016


Baada ya usiku wa March 1 kuchezwa michezo mitano ya Ligi Kuu Uingereza, usiku wa March 2 iliendelea tena michezo ya Ligi Kuu Uingereza, kwa mechi tano nyingine kupigwa katika viwanja mbalimbali Uingereza.
Baadhi ya michezo ya Ligi Kuu Uingereza iliyochezwa usiku wa March 2 ni mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Man City, Arsenal dhidi ya Swansea City na Man United dhidi ya Watford, mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Man City ndio ulikuwa unatazamwa kwa kiasi kikubwa.
31C8C7E600000578-3473554-image-m-10_1456952641157
Man City ambao walikuwa ugenini katika uwanja wa Anfield, walikubali kipigo cha goli 3-0, Magoli ya Adam Lallana dakika ya 34, James Milner dakika ya 31 na Roberto Firmino dakika ya 57 yalitosha kuimaliza Man City ndani ya Anfield.
Kipigo hicho kimewafanya Man City wabaki nafasi ya nne wakiwa na point 47 katika michezo ya 28, wakati Liverpool wakiwa nafasi ya nane katika Ligi na wametimiza jumla ya point 41 baada ya ushindi huo wakiwa michezo sawa na Man City.
Matoke ya mechi za Ligi Kuu Uingereza March 2 
  • Arsenal 1 – 2 Swansea City
  • Stoke City 1 – 0 Newcastle United
  • West Ham United 1 – 0 Tottenham Hotspur
  • Liverpool 3 – 0 Manchester City
  • Manchester United 1 – 0 Watford

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More