Sunday, March 20, 2016

DR.SHEIN AWEKA MATUMAINI YA KUSHINDA KWA KISHINDO



Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed alizungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera kisiwani Unguja  ambapo alisema anaamini atashinda kwa kishindo na kuhusu kushindwa  alisema tusubiri matokeo ya uchaguzi ndiyo yataamua.


"Nimepata nafasi ya kupiga kura kama haki yangu ya  kimsingi na kumekuwa na utulivu mkubwa kwenye zoezi hili,hali ya ulinzi imeimarishwa.


"Matumaini yangu ni kushinda kwa kishindo, kuhusu kushindwa ndugu muandishi tusubiri matokeo ndiyo yataamua".Alisema Dkt. Ali MohammedShein

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More