Sunday, March 20, 2016

Diamond Platnumz Ametoa Sababu za Wasanii Wakubwa Afrika Kupotea Kwenye Ramani ya Muziki...


Diamond Platnumz ametoa sababu ambazo anaimani zinasababisha wasanii wakubwa AFrika kupotea kwenye ramani ya muziki na kusema ni kuendekeza mashauzi, starehe na kutaka kujionesha.

“Unajua wasanii wengi wanapoteza na kushuka kimuziki sababu ya starehe pamoja na mashauzi. Unakuta mtu amepata mafanikio kidogo anaanza mashauzi na kufanya starehe zisizo na tija, ndiyo maana mimi huwezi kuniona kwenye starehe hata wasanii wa WCB ni hivyo hivyo”

Diamond amempa shavu Shettah kwa kusema ni mfani mzuri wa kuigwa

“Mimi namkubali sana Shettah kwani jamaa ni bahili sana anaweza kutoka kufanya show na akakwambia sina pesa, hata gari yake aliyonunua juzi amenunua kwa pesa zake sababu anakusanya pesa zake na kufanyia vitu vya msingi. Sasa hivi Shettah anajenga nyumba yake na hiyo yote sababu si mtu wa mashauzi na wala si mtu wa starehe”

Diamond alifanyiwa mahojiano wakati anamtambulisha RayMond

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More