Thursday, April 23, 2015

WENGER AKIRI KUCHEMKA KUMUUZA FABREGAS.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekiri kujuta kumruhusu Cesc Fabregas kuondoka lakini amewataka mashabiki wa timu hiyo kumuheshimu kiungo huyo wa Chelsea pindi watakapocheza nao katika Uwanja wa Emirates Jumapili hii. Fabregas mwenye umri wa miaka 27 aliondoka Arsenal mwaka 2011 na kwenda Barcelona lakini baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza alirejea katika Ligi Kuu kiangazi mwaka jana chini Jose Mourinho. Akihojiwa Wenger amesema kitu pekee anachojutia in kumuacha kiungo huyo aondoke lakini anachoataka yeye in kila mchezaji aheshimiwe. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa anampongeza Fabregas kwa jinsi alivyoimarika na kuwa mchezaji tegemeo kwa Chelsea msimu huu. Posted by beki3 at 7:59 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest JAPANA KUWA MWENYEJI WA MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA. SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza Japan kuwa mwenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia kea kipindi cha miaka miwili ijayo. Baada ya kuandaa michuano hiyo mara ya mwisho mwaka 2012, Japana inatarajiwa kuwa mwenyeji tena mwaka 2015 na 2016, huku kwa mwaka huu ikitarajiwa kufanyika Desemba 10 mpaka 20. Katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke alithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa Japan imeonyesha weledi mkubwa katika kuandaa michuano ya FIFA, zikiwemo fainali sita za Klabu Bingwa ya Dunia ambazo zimekuwa na mafanikio. Naye rais wa Chama cha Soka cha Japan-JFA, Kuniya Daini amesema nafasi hiyo ni nyingine ya kipekee kea wachezaji na mashabiki kushuhudia michuano mikubwa ya soka ya vilabu. JFA inatarajia kutangaza miji itakayotumika kwa ajili ya michuano hiyo ya siku 10 baadae ambapo bingwa mtetezi in mabingwa wa Ulaya Real Madrid. Posted by beki3 at 7:58 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest FULANA YAMPONZA GUARDIOLA. SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limemfungulia mashitaka meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kea kuvaa fulana yenye maandishi ya kudai haki ya mwandishi wa habari za michezo aliyeuawa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana. Mwanahabari huyo Jorge Lopez alifariki baada ya teksi aliyokuwa amepanda akielekea hotelini kwake kugongwa na gari linalodaiwa kuwa lilikuwa limeibwa katikati ya jiji la Sao Paulo nchini Brazil mwaka jana. Guardiola alikuwa amevaa fulana yenye maandishi ya kudai haki ya uchunguzi wa kifo cha mwandishi huyo wakati wa mkutano wake na wanahabari kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto juzi. UEFA imesema kwamba Guardiola amechukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu kitendo alichofanya hakihusiani na masuala ya michezo. Kanuni za shirikisho hilo zinapiga marufuku kea mtu yeyote kutumia matukio ya kimichezo kwa shughuli zisizohusiana na suala hilo. Posted by beki3 at 7:57 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest KUSHUHUDIA PAMBANO LA MAYWEATHER NA PAQUIAO MILIONI 18. TIKETI kwa ajili ya pambano langumi la wiki ijayo kati ya bondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao hatimaye zinatarajiwa kuingia sokoni leo huku zikitegemwa kugharimu kiasi cha paundi 60,000. Ukumbi wa MGM Grand uliopo jijini Las Vegas, Nevada una uwezo wa kuingoza watazamaji 16,500 lakini in tiketi 1,000 pekee ndio zitakwenda sokoni. Tiketi zilizobakia zitakakwenda kwa mabondia wenyewe, casino, wadhamini na mapromota wa pambano hilo. Tiketi rahisi zaidi katika pambano hilo la Mei 2 mwaka huu zinatarajiwa kugharimu kiasi cha paundi 1,000 kwa pesa za madafu shilingi 2,903,000 na kupanda mpaka paundi 6,700 sawa na shilingi 18,869,500. Mayweather raia wa marekani ataingia katika pambano hilo akiwa na rekodi ya kushinda mapambano yake yote 47 ya kulipwa aliyocheza 26 kati ya hayo akishinda kea knockout wakati Pacquiao raia wa Filipino akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 57, kupoteza matano na sare mawili. Posted by beki3 at 7:56 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest JUVENTUS YAKIRI KUANZA MAZUNGUMZO YA KUMSAJILI DYBALA. OFISA mkuu wa Juventus Giuseppe Marotta amethibitisha kuwa klabu hiyo iko katika mazungumzo na Palermo kea ajili ya kumsajili mshambuliaji Paulo Dybala lakini akaongeza kuwa dili hilo bado in gumu kufanikiwa. Dybala amekuwa katika kiwango bora msimu huu akiwa amefunga mabao 13 katika michezo 30 aliyoichezea Palermo jambo ambalo limemfanya kuzivutia klabu kadhaa zikiwemo Inter Milan, Arsenal na Chelsea. Wakala wa mchezaji huyo tayari amedai kuwa Chelsea wametoa ofa ya euro milioni 41, huku Juventus nao wakitaka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji baada ya Carlos tevez kudaiwa kutaka kurejea nyumbani kwao Argentina katika klabu ya Boca Juniors. Marotta amesema wanazungumza na rais wa Palermo Maurizio Zamparini lakini mazungumzo hayo yanaonekana kuwa magumu kutokana na rais huyo kutaka kitita cha euro milioni 50 kea ajili ya kumuachia nyota huyo. Posted by beki3 at 7:53 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest BAYERN NAO WAMNYEMELEA IVANOVIC WA CHELSEA. KLABU ya Bayern Munich iko tayari kuongeza nguvu zake kea ajili ya kumuiba Branislav Ivanovic kutoka Chelsea katika majira ya kiangazi. Beki huyo wa kimataifa wa Serbia amebakisha mkataba wa mwaka mmoja Stamford Bridge na mabingwa hao wa Bundesliga wameungana na Paris Saint-Germain kufuatilia maendeleo ya mustabali wa mchezaji huyo kea karibu. Ivanovic amepewa ofa ya kuongezwa mkataba wa mwaka mmoja kama sera za timu hiyo zinavyotaka kwa wachezaji waliozidi umri wa miaka 30 lakini bado hajakubali kusaini. Beki huyo amekuwa tegemeo kea Chelsea toka alipojiunga nao kea kitita cha paundi milioni 9.5 akitokea klabu ya Lokomotiv Moscow ya Urusi mwaka 2008.

WENGER AKIRI KUCHEMKA KUMUUZA FABREGAS. MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekiri kujuta kumruhusu Cesc Fabregas kuondoka lakini amewataka mashabiki wa timu hiyo kumuheshimu kiungo huyo wa Chelsea pindi watakapocheza nao katika Uwanja wa Emirates Jumapili hii. Fabregas mwenye umri wa miaka 27 aliondoka Arsenal mwaka 2011 na kwenda Barcelona lakini baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza alirejea katika Ligi Kuu kiangazi mwaka jana chini Jose Mourinho. Akihojiwa Wenger amesema kitu pekee anachojutia in kumuacha kiungo huyo aondoke lakini anachoataka yeye in kila mchezaji aheshimiwe. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa anampongeza Fabregas kwa jinsi alivyoimarika na kuwa mchezaji tegemeo kwa Chelsea msimu huu. Posted by beki3 at 7:59 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest JAPANA KUWA MWENYEJI WA MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA. SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limetangaza Japan kuwa mwenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia kea kipindi cha miaka miwili ijayo. Baada ya kuandaa michuano hiyo mara ya mwisho mwaka 2012, Japana inatarajiwa kuwa mwenyeji tena mwaka 2015 na 2016, huku kwa mwaka huu ikitarajiwa kufanyika Desemba 10 mpaka 20. Katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke alithibitisha taarifa hizo na kudai kuwa Japan imeonyesha weledi mkubwa katika kuandaa michuano ya FIFA, zikiwemo fainali sita za Klabu Bingwa ya Dunia ambazo zimekuwa na mafanikio. Naye rais wa Chama cha Soka cha Japan-JFA, Kuniya Daini amesema nafasi hiyo ni nyingine ya kipekee kea wachezaji na mashabiki kushuhudia michuano mikubwa ya soka ya vilabu. JFA inatarajia kutangaza miji itakayotumika kwa ajili ya michuano hiyo ya siku 10 baadae ambapo bingwa mtetezi in mabingwa wa Ulaya Real Madrid. Posted by beki3 at 7:58 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest FULANA YAMPONZA GUARDIOLA. SHIRIKISHO la Soka la Ulaya-UEFA limemfungulia mashitaka meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kea kuvaa fulana yenye maandishi ya kudai haki ya mwandishi wa habari za michezo aliyeuawa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana. Mwanahabari huyo Jorge Lopez alifariki baada ya teksi aliyokuwa amepanda akielekea hotelini kwake kugongwa na gari linalodaiwa kuwa lilikuwa limeibwa katikati ya jiji la Sao Paulo nchini Brazil mwaka jana. Guardiola alikuwa amevaa fulana yenye maandishi ya kudai haki ya uchunguzi wa kifo cha mwandishi huyo wakati wa mkutano wake na wanahabari kabla ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto juzi. UEFA imesema kwamba Guardiola amechukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu kitendo alichofanya hakihusiani na masuala ya michezo. Kanuni za shirikisho hilo zinapiga marufuku kea mtu yeyote kutumia matukio ya kimichezo kwa shughuli zisizohusiana na suala hilo. Posted by beki3 at 7:57 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest KUSHUHUDIA PAMBANO LA MAYWEATHER NA PAQUIAO MILIONI 18. TIKETI kwa ajili ya pambano langumi la wiki ijayo kati ya bondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao hatimaye zinatarajiwa kuingia sokoni leo huku zikitegemwa kugharimu kiasi cha paundi 60,000. Ukumbi wa MGM Grand uliopo jijini Las Vegas, Nevada una uwezo wa kuingoza watazamaji 16,500 lakini in tiketi 1,000 pekee ndio zitakwenda sokoni. Tiketi zilizobakia zitakakwenda kwa mabondia wenyewe, casino, wadhamini na mapromota wa pambano hilo. Tiketi rahisi zaidi katika pambano hilo la Mei 2 mwaka huu zinatarajiwa kugharimu kiasi cha paundi 1,000 kwa pesa za madafu shilingi 2,903,000 na kupanda mpaka paundi 6,700 sawa na shilingi 18,869,500. Mayweather raia wa marekani ataingia katika pambano hilo akiwa na rekodi ya kushinda mapambano yake yote 47 ya kulipwa aliyocheza 26 kati ya hayo akishinda kea knockout wakati Pacquiao raia wa Filipino akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 57, kupoteza matano na sare mawili. Posted by beki3 at 7:56 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest JUVENTUS YAKIRI KUANZA MAZUNGUMZO YA KUMSAJILI DYBALA. OFISA mkuu wa Juventus Giuseppe Marotta amethibitisha kuwa klabu hiyo iko katika mazungumzo na Palermo kea ajili ya kumsajili mshambuliaji Paulo Dybala lakini akaongeza kuwa dili hilo bado in gumu kufanikiwa. Dybala amekuwa katika kiwango bora msimu huu akiwa amefunga mabao 13 katika michezo 30 aliyoichezea Palermo jambo ambalo limemfanya kuzivutia klabu kadhaa zikiwemo Inter Milan, Arsenal na Chelsea. Wakala wa mchezaji huyo tayari amedai kuwa Chelsea wametoa ofa ya euro milioni 41, huku Juventus nao wakitaka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji baada ya Carlos tevez kudaiwa kutaka kurejea nyumbani kwao Argentina katika klabu ya Boca Juniors. Marotta amesema wanazungumza na rais wa Palermo Maurizio Zamparini lakini mazungumzo hayo yanaonekana kuwa magumu kutokana na rais huyo kutaka kitita cha euro milioni 50 kea ajili ya kumuachia nyota huyo. Posted by beki3 at 7:53 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest BAYERN NAO WAMNYEMELEA IVANOVIC WA CHELSEA. KLABU ya Bayern Munich iko tayari kuongeza nguvu zake kea ajili ya kumuiba Branislav Ivanovic kutoka Chelsea katika majira ya kiangazi. Beki huyo wa kimataifa wa Serbia amebakisha mkataba wa mwaka mmoja Stamford Bridge na mabingwa hao wa Bundesliga wameungana na Paris Saint-Germain kufuatilia maendeleo ya mustabali wa mchezaji huyo kea karibu. Ivanovic amepewa ofa ya kuongezwa mkataba wa mwaka mmoja kama sera za timu hiyo zinavyotaka kwa wachezaji waliozidi umri wa miaka 30 lakini bado hajakubali kusaini. Beki huyo amekuwa tegemeo kea Chelsea toka alipojiunga nao kea kitita cha paundi milioni 9.5 akitokea klabu ya Lokomotiv Moscow ya Urusi mwaka 2008. Posted by beki3 at 7:52 AM No comments: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Older Posts Home Subscribe to: Posts (Atom) Search This Blog

Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More