Wednesday, May 13, 2015

JUA HAPA KUHUSU GARI MPYA YA MIZIGO INAYO JIONGOZA YENYEWE...ANGALIA VIDEO YAKE HAPA

G1 
Imetokea kwenye jimbo la Nevada Marekani ambako Freightliner walipewa kibali cha kulifanyia majaribio gari la mizigo ambalo lina uwezo wa kujiongoza lenyewe na kumpa dereva nafasi ya kupumua kidogo.
Tofauti na magari mengine ambayo yanaweza kujiendesha yenyewe, hili ni lazima dereva awepo pembeni kama kawaida ila akishaliruhusu kujiendesha lenyewe anaweza kuendelea na kazi zake za pembeni kama kupanga safari zijazo na mengine ya kawaida lakini anakua macho kwa kinachoendelea barabarani kama inavyoonekana kwenye picha ya kwanza.
Ni gari ambalo linaweza kujiongoza kwa msaada wa Radar sensors and cameras ambapo japo hawajasema muda kamili wa gari hili kuanza kufanya kazi, imeripotiwa kwamba haitachukua muda mrefu kuingia barabarani.
Freightliner inamilikiwa na Daimler AG ambao pia ndio wanahusika kutengeneza magari ya kifahari ya Mercedes-Benz
Mercedes-Benz

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More