Hii sio taarifa nzuri kwa fans wa Brazil baada ya staa wao Neymar kupunguzwa kenye Kikosi cha Timu hiyo.
Neymar
amefungiwa mechi nne kutokana na utovu wa nidhamu Uwanjani ambapo
alichukua mpira na kumpiga nao mgongoni Mchezaji wa Colombia, Pablo Armero ambapo katika mechi hiyo Brazil walifungwa 1-0.
Neymar alioneshwa kadi nyekundu na hukumu ya kwanza iliyotolewa ilikuwa Neymar
akose mechi moja tu, lakini baadae Shirikisho la Soka Amerika Kusini
walipitia upya kesi yake na kumwongezea adhabu na kumfungia mechi nne
baada ya kugundua alitoa kauli mbaya kwa mwamuzi Enrique Osses.
Staa wa Colombia, Carlos Bacca nae kafungiwa kucheza mechi mbili lakini Shirikisho hilo limesema milango iko wazi kama jamaa wakiamua kukata rufaa
0 comments:
Post a Comment