Saturday, April 4, 2015

SUMA LEE KUACHANA NA MUZIKI



Msanii aliyefanya vizuri na single ya ‘Hakunaga’, Suma Lee amesema hatofanya tena muziki kwa sababu ameachana kabisa na maisha hayo.

Suma ambaye alitengeneza pesa nyingi kupitia hit yake ya ‘Hakunaga’, amesema hana mpango wa kuzitoa nyimbo zake zilizoko studio ambazo hazijatoka.

“Sifanyi tena muziki na nimeachana kabisa na maisha hayo, na nyimbo zote zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke baada ya kuzilipia, “ Alisema Suma.

“Kuna wimbo mmoja nimefanya na Cp ambao ndio ulikuwa wa kurudisha kundi la Parklane, pia nimeuzuia, labda Cp auchukue yeye.

Kilichobaki ni kuwaombea wazazi wetu waliotutangulia, wengine walikuwa hawata ki tufanye kazi hizi, kwa kuwa hawapo na hakuna wakutukataza tena, bora tukae na kuwaombea.”

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More