Hii ni hadithi inayo husu utamu na machungu aliyo yapitia kijana brian katika maisha yake,ikiwa
huu ni mwanzo,mi nikiwa mtunzi nakuomba ufuatilie kwa makini hadithi hii mpaka
mwisho kwani ina mafundisho na ya kusisimua
pia huenda mawili au matatu yaliyo mtokea brian yasha wahi kuku tokea wewe au
jamaa yako wa karibu..utajifunza jinsi ya kuya kabiri..huyu hapa brian
……brian baada ya kumaliza darasa la saba kijijini kwao bigwa
mkoani morogoro na kuto fanikiwa kufaulu kuendelea na masomo ya sekondari,mwaka
wa kwanza alijishughulisha na shughuli za shambani kwa muda wa mwaka mmoja,kwa
kuwa alikuwa mchapa kazi ali fanikiwa kupata mavuno ya kutosha hivyo kupata
mtaji wa kufanya biashara..aliweza kusafirisha mazao yake mjini ambako alipata
kujua vyema ni jinsi gani wale walio kuja kununua bidhaa zao kijijini na
kuzipeleka mjini wali pata faida zaidi ya wao wenyewe wakulima
Alicho kifanya badala ya kuendelea kulima akawa anakuja
kununua maazo na kupeleka mjini kuuuza na kweli ali fanikiwa kupapata kiasi cha
kuweza kupanga chumba huko mjini na kuanza maisha huko mjini,katika pilika
pilika zake ali kutana na jamaa ambaye alisoma nae ambaye anaitwa benson,na
waka kumbushana mambo mengi ya shule,mpaka kufikia benson kumu ahidi ata
mkutanisha na mwalimu wa boxing kwani ukiacha kusoma tu kwenye michezo brian
alikuwa mzuri sana katika masuala ya ubondia hivyo benson ali mshauri japo
umefeli shule jaribu na huu upande mwingine.
Kama alivyo mu ahidi benson ali mkutanisha mr.lazaro ambaye
ana sehemu maalum ya kujifunza michezo mbalimbali,hivyo brian ali anza mazoezi
na kwakuwa alikuwa na kipaji muda sio muda jina lake lika anza kuwa kubwa,na
ali pigana mapambano mengi kiasi cha kufikia kupata mapambano ya kimataifa na
kushinda,hivyo alikuwa mtu maarufu kwa kipindi kifupi sana…
Ilikuwa kawaida sana kuenda kumtembelea benson shuleni kwao
kila ifikapo weekend na kumuachia chochote kwani kidogo alikuwa na kipato kwani
alikuwa aki ingiza pesa katika mapambano ambayo ali kuwa ana pigana.
Siku moja kama ilivyo kawaida brian alipo enda
kumtembelea benson alikuta ndio siku wanayo funga shule hivyo baada ya kumaliza
hatua zote za kufunga shule wali itumia siku hiyo kuenda club na ku enjoy,na
siku hiyo club ya supersub djs ilijaa wana funzi kibao maana ni siku ambayo
walifunga shule,hapo benson ali jisikia fahari kuwa karibu na mtu
maarufu(brian) na kuwa tambulisha wanafunzi wenzake….
Pia hapo ndipo benson akatumia fulsa hiyo kumtabulisha
Winnie ambaye ni girlfriend wake,pia Lydia ambaye ni rafiki wa Winnie,bila
kushangaa Lydia alijisogeza karibu na brian baada ya kugundua ni mtu
maarufu,hivyo hapo hapo ndio ukwa mwanzo wa mahusiano kati brian na
lydia...
mahusiano hayo yali dumu kwa siri huku brian akiendelea na
shughuli yake ya michezo huku Lydia akiwa shuleni mpaka lydia alipo malizqa
kidato cha sita na kuanza chuo kikuu hapo ndipo brian sasa alitangaza hadharani
mpaka magazetini kuwa mchumba wake ambaye ata muoa ni Lydia
Kipindi hicho Lydia yuko chua alikuwa na na rafiki mwingine
uki acha Winnie kwani walichaguliwa vyuo tofauti,huyo rafiki yake alikuwa
akiitwa lucy,pia alikuwa mrembo sana na alionekana kujiamini sana katika
maongezi yake lakini alimuheshimu sana shemeji yake brian,kwa kuwa brian
alipanga ilikuwa ni kawaida siku za weekend Lydia na lucy kuenda kumtembelea
brian…
Siku moja wakiwa chuoni Lydia na lucy ghafla hali ya Lydia
ika badilika na kuwa sio nzuri,Lydia ali lala mika na kusema anahisi maumivu
makali ya kichwa na misuli kwa ujumla,maamuzi walio fikia ni kwamba ili kupata
uangalizi mzuri inabidi Lydia arudi nyumbani kwao,waka mpigia simu brian na
kumueleza aka waambia wapiti kwake ili awapatie pesa kidogo..
Wakachukua taxi na kupitia kwa brian waka ingia ndani na
baada ya Lydia kumuona brian akadai anataka kupunzika kidogo hivyodereva wa
taxi akalipwa na kuondoka,lucy akaingia jikoni na kuandaa chaukula wakala,brian
aka muuliza Lydia hali yake na akjibu sio mbaya naweza vumilia mpaka kesho,lucy
aka aga na kurudi chuoni kwao.
Baada ya mida ya saa saba usiku hali ya Lydia ikwa mbaya
tena,brian akachua vidonge ambavyo ni vya kupunguza maumivu ambavo ali wahi
kuvitumia wakati Fulani na kumpatia Lydia ili vimsaidie mpaka hasubuhi,ndipo waende
hospitali,kweli baada ya muda Lydia alipata usingizi waka lala..ilipo fika
hasubuhi brian ali amka mapema kuandaa maji ya moto kwaajili ya Lydia
kuoga,kasha anywe chai waweze kuenda hospitali
Kila kitu kilipo kuwa tayari brian ali muamsha Lydia bila mafanikio
kwani Lydia alikuwa tayari amesha kata roho muda mrefu sana,hakuwa ame pata
nafuu alipo lala na wala haukua usingizi,dakika chache tu baada ya kutumia vile
vidonge alilala moja kwa moja…haya ndugu msomaji,kipi kilicho mu ua Lydia ni
kuzidiwa nahoma ,au ni vidonge alivyopewa na brian…
Kama kweli nini kita mtokea brian atashitakiwa ama
itakuwaje?usikose kusoma sehemu ifuatayo ya hadithi yako tamu….tamu na chungu
Namimtunzi wako…BRIAN GERVARCE
0 comments:
Post a Comment