Saturday, April 4, 2015



       
TAMU NA CHUNGU…SEHEMU YA 1
Hii ni hadithi inayo husu utamu na machungu aliyo  yapitia kijana brian katika maisha yake,ikiwa huu ni mwanzo,mi nikiwa mtunzi nakuomba ufuatilie kwa makini hadithi hii mpaka mwisho kwani  ina mafundisho na ya kusisimua pia huenda mawili au matatu yaliyo mtokea brian yasha wahi kuku tokea wewe au jamaa yako wa karibu..utajifunza jinsi ya kuya kabiri..huyu hapa brian
……brian baada ya kumaliza darasa la saba kijijini kwao bigwa mkoani morogoro na kuto fanikiwa kufaulu kuendelea na masomo ya sekondari,mwaka wa kwanza alijishughulisha na shughuli za shambani kwa muda wa mwaka mmoja,kwa kuwa alikuwa mchapa kazi ali fanikiwa kupata mavuno ya kutosha hivyo kupata mtaji wa kufanya biashara..aliweza kusafirisha mazao yake mjini ambako alipata kujua vyema ni jinsi gani wale walio kuja kununua bidhaa zao kijijini na kuzipeleka mjini wali pata faida zaidi ya wao wenyewe wakulima
Alicho kifanya badala ya kuendelea kulima akawa anakuja kununua maazo na kupeleka mjini kuuuza na kweli ali fanikiwa kupapata kiasi cha kuweza kupanga chumba huko mjini na kuanza maisha huko mjini,katika pilika pilika zake ali kutana na jamaa ambaye alisoma nae ambaye anaitwa benson,na waka kumbushana mambo mengi ya shule,mpaka kufikia benson kumu ahidi ata mkutanisha na mwalimu wa boxing kwani ukiacha kusoma tu kwenye michezo brian alikuwa mzuri sana katika masuala ya ubondia hivyo benson ali mshauri japo umefeli shule jaribu na huu upande mwingine.
Kama alivyo mu ahidi benson ali mkutanisha mr.lazaro ambaye ana sehemu maalum ya kujifunza michezo mbalimbali,hivyo brian ali anza mazoezi na kwakuwa alikuwa na kipaji muda sio muda jina lake lika anza kuwa kubwa,na ali pigana mapambano mengi kiasi cha kufikia kupata mapambano ya kimataifa na kushinda,hivyo alikuwa mtu maarufu kwa kipindi kifupi sana…
Ilikuwa kawaida sana kuenda kumtembelea benson shuleni kwao kila ifikapo weekend na kumuachia chochote kwani kidogo alikuwa na kipato kwani alikuwa aki ingiza pesa katika mapambano ambayo ali kuwa ana pigana.
   Siku moja kama ilivyo kawaida brian alipo enda kumtembelea benson alikuta ndio siku wanayo funga shule hivyo baada ya kumaliza hatua zote za kufunga shule wali itumia siku hiyo kuenda club na ku enjoy,na siku hiyo club ya supersub djs ilijaa wana funzi kibao maana ni siku ambayo walifunga shule,hapo benson ali jisikia fahari kuwa karibu na mtu maarufu(brian) na kuwa tambulisha wanafunzi wenzake….
Pia hapo ndipo benson akatumia fulsa hiyo kumtabulisha Winnie ambaye ni girlfriend wake,pia Lydia ambaye ni rafiki wa Winnie,bila kushangaa Lydia alijisogeza karibu na brian baada ya kugundua ni mtu maarufu,hivyo hapo hapo ndio ukwa mwanzo wa mahusiano kati brian na lydia,lakini je si unajua Lydia bado ni mwanafunzi? Unataka kujua nini kita mkuta brian,usikose kusoma sehemu ya pili ya hadithi hii tamu na chungu
Na mtunzi wako BRIAN GERVARCE CHONDOMA

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More