Sunday, March 29, 2015

Yako mengi Duniani, na hii simu iliyotengenezwa kwa majani umeipata?



Teknolojia inatufungulia mapya kila siku.. Nakumbuka simu za kwanza za mkononi zilikuwa kubwa halafu nzito, baadae ikaja fashion ya simu ndogo ndogo, zile kubwa watu wakawa wanaziita ‘mshindi’ ambalo ni jina la sabuni… Sasa hivi tunaona fashion ya simu kubwa inarudi mdogomdogo.
Sean Miles anaingia kwenye historia, anaingia kwenye headlines pia.. yeye kagundua hii simu ambayo imetengenezwa kwa majani kabisa pamoja na mchanganyiko wa vitu vingine vilivyochakaa ama vilivyoharibika.
O2-recycle-grass-phone-designboom03Dili ambayo alipewa na Kampuni ya O2 ilikuwa Miles afanye ubunifu njia ambayo wataweza kutumia mabaki ya vitu ambavyo vimechakaa na havifai kwa matumizi, katoka na hii ambayo hata waliomuagiza hiyo kazi imewashangaza yani.
Unaambiwa cover ya simu hii ukiiangalia ni kama majani kabisa.
_81927339_grassphone2Ubunifu huu umefungua ukurasa mpya kwenye Teknolojia, Kampuni ya O2 wanaangalia kama wataweza kuweka nguvu nyingi zaidi ili simu zenye cover hizi zilizotengenezewa majani zitengenezwe nyingi na kuingia kwenye soko la Dunia.
O2-Grass-Phone-31-537x444
Vipi mtu wangu ukikutana na hii simu pale Kariakoo an Mlimani City kuna kitu kitakufanya usiipende labda?
Bonyeza play umcheki Sean Miles akifanya kazi yake sasa kuitengeneza hii simu…


0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More