MWIGIZAJI mahiri katika tasnia ya filamu na Komedi Salma Jabu ‘Nisha’
amedai kuwa ana kazi kubwa katika kulinda nafasi yake ya uigizaji bora
wa Komedi na ustadi katika kutengeneza kazi zake na ziendelee kuwa bora
ili asipotee na kuonekana kama alibahatisha.
“Wahenga husema kuwa ni rahisi kupata nafasi ya kwanza, lakini si
rahisi kuilinda hivyo name lazima niilinde nafasi yangu niliyoipata
mwaka jana baada ya kuipigania kwa muda mrefu katika tasnia ya filamu na
nitailinda kwa kufanya kazi bora tu,”anasema Nisha.
Msanii huyo anaamini kuwa kwa Bongo si kazi nyepesi kufanya kazi na
kukubalika na wapenzi wa filamu kwani kila siku wasanii wanaongezeka na
kuja katika hali ya ushindani mkubwa ambao kama haujajipanga lazima
upotee katika tasnia ya filamu baada ya kuvuma kwa muda mfupi tu
0 comments:
Post a Comment