Tuesday, March 31, 2015

ANA WATOTO 40 NA BADO ANA MPANGO

babaUzazi wa mpango ni jambo ambalo husisitizwa ndani ya jamii  ili kuwa na familia bora na uwezo wa kutunza familia kutokana na idadi ya watoto wanaozaliwa.

Mike Holpin hakuona umuhimu wala hana habari na uzazi wa mpango kwani licha ya kuwa na watoto 40 bado anafikiria kuongeza wengine huku akiamini hata vitabu vya dini vinaruhusu.

Mwanaume huyo mwenye miaka 56 mwenyeji wa Monmuothshire, Uingereza alipata mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka 19 tu na kwa sasa mtoto wake wa kwanza ana miaka 37 huku wa mwisho akiwa na miaka mitatu.

mgongoWatoto hao amezaa na wanawake 20 tofauti na amesisitizi yupo tayari kuongeza wengine kwani hata vitabu vya dini vimeruhusu na ameamua kujichora tattoo yenye majina ya watoto wake ili aweze kuwakumbuka.

Aliongeza kati ya wanawake 20 aliowazalisha sita ndio aliweza kuishi nao lakini baadae alitengana nao kutokana na tabia yake ya kutokuwa mwaminifu pamoja na kuwanyanyasa.

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More