Friday, May 1, 2015

MAKOCHA NA MAAMUZI YAO KUHUSU HUYU STRAIKER FUNDI


ngasa
Jopo maalum la makocha ambao hutafuta wachezaji bora kwa kila mchezo kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara wametoa matokeo ya wachezaji waliochaguliwa kuwa bora zaidi ya wenzao kwenye ligi hiyo kwa mwezi April.
Mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa, Mrisho Ngasa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom ya mwezi Aprili kufuatia kuwashinda wachezaji wenzake Amos EdwardFrank Domayo na Emmanuel Okwi baada ya kupata alama nyingi za mchezaji bora kwa kila mchezo.
Mbali na Ngassa pia James Ambrose nae amefanikiwa kushinda nafasi hiyo.
James Ambrose na Mrisho Ngasa watazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodaom.

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More