Monday, April 20, 2015

TAMU NA CHUNGU SEHEMU YA 2

story na brian gervarce

   na wakati mgumu baada ya lydia kufariki akiwa kwake,baada ya kumuamsha kwa muda bila mafanikio aka gundua tayari amesha fariki,aka chukua hatua ya kupiga simu polisi kutoa taarifa,punde polisi walifika na kuchukua mwili wa marehemu kuupeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi,hivyo brian naye ali bebwa na kuwekwa chini ya ulizi akisubiri uchunguzi wa daktali ili kugundua chanzo kilicho sababisha kifo cha lydia..
baada ya majibu ya daktari kutoka,brian ana jikuta na wakati mgumu sana  kwani iligundulika kwamba lydia alikufa kwa kula chakula chenye sumu,lakini mimi nawewe tuna fahamu wazi kwamba haikuwa sumu bali ni vile vidonge alivyo pewa na brian vilikuwa vimeisha muda wake (expire),hivyo polisi ina mfungulia kesi ya mauaji hivyo anachukuliwa na kupelekwa mahabusu ya gereza la mwana ukome akisubiri siku ya kusikilizwa kwa kesi yake.
brian akiwa ha amini macho yake anajikuta  mahabusu huku akiwa na machungu ya kuondokewa na kipenzi chake ambaye ndio hasa ali tamani kumu oa na kuishi nae katika maisha yake yote yaliyo salia,huku u raiani mazishi ya lydia yanafanyika bila brian kupewa hata ruksa ya kuhudhuria mazishi ya mpenzi wake,yaani ni kipindi ambacho brian ana jikuta na matatizo mfululizo kwani bila kujua kwamba brian ni bondia,mbabe mmoja mule mahabusu ana mletea brian vurugu na brian kwa hasira ana mtandika ngumi kali na yule jamaa anadhirahi palepale.
askari wakasikia vurugu na wanapo ufungua mlango wa mahabusu wana kuta mtu akiwa sakafuni amepoteza fahamu,baada ya kuhoji kilicho tokea wana gundua brian  ndiye aliye mtandika yule jamaa(askari...DUHU HIVI WEWE UNA KESI MBICHII,LEOLEO UNA UA MTU MWINGINE?KWELI UTA OZEA JELA WEWE)yule jamaa anachukuliwa na kukimbizwa hospitali,na kupimwa akagundulika amepta mpasuko katika fuvu la kichwa hivyo akaingizwa chumba cha watu mahututi.
kilichofuata brian anawekwa kwenye chumba cha peke yake kwani ki ukweli alikuwa kama ame changanyikiwa,ana pigwa virungu vya kutosha na kutupwa kwenye chumba cha giza akiwa peke yake,brian anawaza kujinyonga lakini ghafla ana kumbuka kilicho mfanya awe pale sio kusudio lake,hivyo ana jipa moyo na kusema MUNGU NAOMBA NIPIGANIE VITA HIVI,KWANI WE NDIO SHAHIDI NA JAJI WA KWELI KUHUSU HILI,SIJA MU UA LYDIA MUNGU WAJUA HILO..
haya ndugu msomaji unataka kujua nini kita endelea?fuatana na mimi katika sehemu ijayo...

0 comments:

Post a Comment

Share

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More