Kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko aliibuka Mchezaji bora wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa
mwezi Desemba 2015. Mzimbabwe huyo aliibuka baada ya kumshinda mchezaji
mwenzake wa Yanga, mshambuliaji Amiss Tambwe, raia wa Burundi.
Kampuni ya simu za mkononi, Vodacom Tanzania, wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara jana walimkabidhi kitita cha Tsh Milioni 1 Kamusoko. Kamusoko
aliisadia timu yake ya Yanga kupata ushindi katika michezo iliyochezwa
mwezi Desemba kwa kushiriki dakika zote katika mechi tatu zilizochezwa
mwezi huo.
Makabidhiano hayo yalifanywa na Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya
wakati timu hiyo ikifanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kujiandaa na mechi yao ya Jumamosi dhidi ya APR ya Rwanda Ligi ya
Mabingwa Afrika.
Kamusoko ameishukuru kampuni ya Vodacom Tanzania
kwa kudhamini Ligi Kuu na kumuwezesha kuonesha kipaji chake pia kwa
kumkabidhi zawadi ya Fedha. Kamusoko amewashukuru pia mashabiki wa timu
yake kwa kuendelea kuwasapoti wachezaji na amesema anawapenda na
anawaamini sana.
0 comments:
Post a Comment