Tofauti zinazo jitokeza hivi karibuni kati ya Wasanii hao wawili yatujia vigumu kabisa kujua kiini chake.
Kwanza ifahamike kwamba Wote wawili ni Majirani, wanaishi JIJINI KINSHASA kwenye Mitaa ya kifahari mahala panapo julikana kwa jina la ” Montfleury “.
Yasemekana Mzozo wa siku hizi Umeibuka kutokana na kitendo cha JB MPIANA kushindwa kumpa Mualiko Jirani yake KOFFI OLOMIDE, wakati alipo andaa SHEREHE kabambe yakumhenzi Bintie DAIDA kwa ajili ya B’Day yake Tarehe 14-07-2014, Wakati wapo Wasanii na Watu wengine Maarufu waliopata fursa ya kuudhuria napia kuwa mashahidi wa Tukio hilo ambalo liliacha Gumzo JIJINI KINSHASA. Ntawataja ( WERRASON, ADOLPH DOMINGUEZ, FALLY IPUPA )..
Siku Chache Baadae KOFFI OLOMIDE nae kwa Upande wake,kaandaa SHEREHE kwa Ajili ya B’Day ya Binti yake DIDI-STONE, Ingawa hajatoa mualiko kwa Watu Wengi ukilinganisha na alivyofanya JB MPIANA.
Ingawa JB MPIANA hajasema Chochote, Tumemsikia KOFFI OLOMIDE,kamtupia mwenzie kwa kusema : ” KWAKWELI MIMI NASHINDWA KUWAELEWA KABISA WATU WENGINE, MTU KASHINDWA KABISA KAZI YA MUZIKI,ANACHOKIJUA KWA SASA NI MAJUNGU PEKEE, WALA SI MIMI NILIE MCHUKULIA MKEWE!!! CHUKI YA NINI JAMANI !!! MIMI SIPO HUKO KABISA.
Kwa hapa nakumbushia kidogo, Wakati bado wapo vizuri katika mawasiliano yao, KOFFI OLOMIDE, Tumemsikia akimtolea sifa Nyingi sana JB MPIANA siku ya B’Day yake Tarehe 02-06-2014, Namnukuu : ” TUNAPO CHUNGUZA VIZURI KWENYE KAZI YA MUZIKI INCHINI CONGO,WAPO MA STAA WAWILI,NAO SIWENGINE BALI NI MIMI NA JB MPIANA ).
Hadi kwa wakati huu bado kabisa JB MPIANA wala hajasema lolote !!! SASA NANI KAJAKUWASHA MOTO ?
Mtu ambae kajiingiza kwenye Mzozo huo ni Chizi wa Mfalme WERRASON anaejulikana kwa jina la SANKARA DE KUNTA. Yeye kamkingia Ubavu JB MPIANA,kwa kumtolea khashfa KOFFI OLOMIDE pale alivyo sema kwamba, HUYO MZEE NIMPUUZI TUU WALA HANA LOLOTE, MWACHENI HUYO KAISHA KABISA, KWANZA MADENI YAMEMZIDI HADI KAENDA KUOMBA DENI KWA JB MPIANA, KUIMBE ALIE MWEMA WA WATU KAMGEA DOLA 30.000.
Maneno hayo, yamemkera vibaya sana KOFFI OLOMIDE, Kwenye video nilio iambatanisha na Post hii, MOPAO MOKONZI katoa maneno ya khebei kwakusema : ” SINA LAKUSEMA,MIMI NAWASIKILIZENI TUU, NA KAMA UNALO LAKUONGEA, BASI NENA YALE YALIO NA UKWELI,SI LAZIMA KWAKO WEWE KUJIFICHA MGONGONI MWA MTU MWENGIEN. NTAKUOMBA NENDA KWENYE TV,NA UONYESHE KWA MAANDISHI YANAYO DHIHIRISHA MATAMSHI YA HUYO MSEMAJI WANU, AMBAE KADAI KWAMBA NIMECHUKUA KUTOKA MIKONONI MWAKO PESA. KWELI KAMA WEWE NI MWANAUME WA UHAKIKA, BASI FANYA HIVYO ILI UKWELI UDHIHIRIKE !!
Posted in: Entertainment,Music
0 comments:
Post a Comment